Maonesho ya Kusafiri ya Japan Foundation "Napenda Sushi (I Love Sushi)" Yafanyika (Makumbusho ya Taifa)
2025/9/24

Mnamo Septemba 19, katika hafla ya ufunguzi wa Maonesho ya Kusafiri ya Japan Foundation "Napenda Sushi (I Love Sushi)" yaliyofanyika katika Makumbusho ya Taifa ya Tanzania, Kaimu Balozi wa Japani, Bw. Ueda alitoa hotuba ya ufunguzi.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Dkt. Noel Lwoga, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, ambaye alimwakilisha mgeni rasmi, Mheshimiwa Balozi Dkt. Pindi Chana, Waziri wa Maliasili na Utalii.
Sushi, inayotambulika kama mwakilishi wa vyakula vya Kijapani na kusajiliwa kama urithi usioshikika wa UNESCO, inasemekana kuwa na historia ya zaidi ya miaka 1,000. Maonesho haya yanaelezea historia na utamaduni wa sushi kupitia michoro ya ukiyo-e ya kipindi cha Edo (kama miaka 300 iliyopita), mfano wa kibanda cha sushi, sanamu za sushi na samaki, na uzoefu wa mgahawa wa sushi wa mtandaoni.
Maonesho yamefunguliwa kwa umma katika Makumbusho ya Taifa kama ifuatavyo:
Kipindi cha Maonesho: Septemba 20 (Jumamosi) – Oktoba 10 (Ijumaa) (Saa za ufunguzi zinazingatia ratiba ya makumbusho, kila siku kuanzia saa 3:30 asubuhi hadi saa 12:00 jioni)
Ukumbi: Chumba Maalum cha Maonesho cha Makumbusho ya Taifa (Shaaban Robert St, Dar es Salaam)