Kutunuku Tuzo ya Heshima kwa Mama Frida Tomito, Mkurugenzi wa Shule ya Sakura ya Wasichana ya Sakura

2024/9/30
cheti
nishani
Balozi Misawa alipohudhuria mahafali ya sita ya shule ya sekondari ya wasichana ya Sakura, alikabidhi Tuzo ya Heshima, Nishani ya jua linalochomoza, na miale ya dhahabu na fedha (The Order of the Rising Sun, Gold and Silver Rays) ya Mama Frida Michael Tomito, mkurugenzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Sakura kwa mtoto wake wa kiume. Mama Frida Tomito alitunukiwa tuzo hiyo mwaka 2024 mwezi wa 4 na akafariki dunia mwezi wa 8 mwaka huu.

Ubalozi wa Japani nchini Tanzania unaheshimu sana mchango wake na unatoa salamu za rambirambi kwa familia na marafiki.
conferment
hotuba ya mtoto wa mama Frida