Hafla ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mfalme wa Japani (His Majesty, the Emperor of Japan) (5 Machi 2025)
2025/3/10

Hafla ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mfalme wa Japani (His Majesty, the Emperor of Japan) ilifanyika katika makazi ya Balozi wa Japani tarehe 5 Machi 2025. Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,aliiwakilisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na wageni wapatao 160 kutoka sekta mbalimbali zikiwemo sekta ya umma na binafsi pamoja na wanadiplomasia kutoka nchi nyingine.
Katika ukumbi huo, wageni walipata fursa ya kujifunza Zaidi kuhusu Japani kupitia maonesho ya Msaada wa Japani kwenye Miradi ya Kijamii na Usalama wa Binadamu (KUSANONE: Grant Assistance for Grassroots Human Security Projects (GGHSP)), Miradi ya JICA, Maonesho ya kimataifa jijini Osaka (Expo 2025 Osaka, Kansai), maonesho ya kuadhimisha makubaliano ya urafiki kati ya Jiji la Nagai, Yamagata na Jiji la Dodoma, pamoja na kona ya kujaribu mchezo wa Kendama ambayo inatengenezwa sana jijini Nagai. Wageni pia walipata fursa ya kuonja chakula cha kijapani (Washoku) kilichoandaliwa na mpishi wa Balozi.