Japanese Film Festival (JFF) Africa Tour in Tanzania -- Sherehe ya Filamu za Kijapani 2026--
Screenings will be held at four venues:
- Saturday, 30 May 2026 — Ardhi University, Dar es Salaam
- Saturday, 6 June 2026 — Sokoine University of Agriculture (SUA), Morogoro
- Sunday, 7 June 2026 — University of Dodoma (UDOM), Dodoma
- Saturday, 13 June 2026 — State University of Zanzibar (SUZA), Zanzibar
- A Letter to Momo (2012) — screening at Ardhi University & UDOM
- The Boy and the Beast (2015) — screening at Ardhi University & UDOM
- SUMMER WARS (2009) — screening at SUA & SUZA
- A SAMURAI IN TIME (2024) — screening at SUA & SUZA
Free giveaways will be available for attendees who complete our survey on the day.
Free entry. Open to all. Come and go as you please.
For more information, please visit: JFF Theater website event page
A Letter to Momo (2012, 120 min, Anime)
© 2012 “A Letter to Momo” Film Partners
Unaweza kuwapata hawa goblins warembo nchini Japani!
Filamu ya katuni ya njozi kuhusu msimu wa joto uliojaa maajabu, ambapo msichana mmoja mwenye umri wa miaka 11 aliyepoteza baba yake anajenga urafiki wa furaha na majini watatu wa ajabu.
Momo mwenye umri wa miaka 11 alimpoteza baba yake katika ajali bila kupata msamaha wake baada ya kumwambia maneno makali. Sasa ni wakati wa kuhamia kwenye nyumba ya kale ya familia kilichoko kisiwa cha mbali ambapo muda unaonekana kuwa umesimama: majengo ya kale ya mbao, sehemu takatifu za ibada, mashamba ya matuta... na hakuna maduka makubwa ya kisasa. Mama yake anapoanza kazi, Momo anatumia muda wake akizurura tu, akishindwa kujizoesha maisha yake mapya na watu wa sehemu hiyo.
Bado anajihisi mwenye wasiwasi kuhusu barua ambayo haikuisha iliyoachwa na baba yake. Barua yenye maneno mawili tu: "Mpendwa Momo." Kisha siku moja, Momo anakutana na kundi la majini watatu ambao wanaonekana kama wametoka moja kwa moja kwenye hadithi za kale... Ingawa mwanzoni aliogopa sura zao za ajabu, hatua kwa hatua Momo anaanza kuwa rafiki wa viumbe hao walafi lakini wanaovutia.
Kwa kutumia rangi laini za kipekee za Kijapani zinazounda hali ya utulivu, filamu hii inaonesha uhalisia wa msukosuko wa kihisia wa msichana mdogo: maumivu ya kumpoteza baba yake, kuchanganyikiwa kwa kubadilishiwa mazingira, na upweke wa kutokuwa na mama yake. Usikose densi ya ajabu ya majini hao. Unaweza kujikuta ukiicheza mwenyewe bila hata kujua!
The Boy and the Beast (2015, 119 min, Anime)
©2015 THE BOY AND THE BEAST FILM PARTNERS
Ninaweza kuwa imara nikiwa nawe.
Mvulana mpweke anakutana na Hayawani mwenye nguvu lakini mbinafsi ambaye pia ni mpweke, na hatua kwa hatua wanaunda uhusiano imara unaolingana na uhusiano wa kweli wa baba na mwana.
Filamu ya The Boy and the Beast ni filamu ya katuni ya Kijapani ya mwaka 2015 ya matukio na njozi iliyoandikwa na kuongozwa na HOSODA Mamoru. Siku moja, mvulana mpweke aitwaye Ren anakutana na hayawani mpweke, Kumatetsu, na anaamua kwenda kuishi katika ulimwengu wa hayawani ili awe na nguvu. Anakuwa mwanagenzi wa Kumatetsu, ambaye anampa jina jipya, Kyuta.
Mwanzoni, wanatofautiana kwa kila jambo, lakini maisha yao ya ajabu na mafunzo ya pamoja yanawasaidia wote wawili kukomaa, na hatua kwa hatua uhusiano baina yao unaimarika na kuwa kama ule wa baba na mwana.
Kyuta anapokua na kuwa kijana shupavu, anajikuta amerudi katika ulimwengu wa wanadamu kwa bahati mbaya na anakutana na msichana wa shule, Kaede. Kukutana kwake na Kaede, ambaye anamfundisha kuhusu ulimwengu mpya na maadili yake, kunamfanya aanze ajiulize yeye ni wa ulimwengu gani haswa.
Kisha, jambo muhimu linatokea ambalo linahusisha ulimwengu wa wanadamu na ulimwengu wa hayawani. Wakati unawadia kwa kila mmoja wao kufanya maamuzi yake mwenyewe.
SUMMER WARS (2009, 114 min, Anime)
©2009 SUMMERWARS FILM PARTNERS
Mpendwa aliyenivutia, kazi mpya ya muda, na vita mpya kabisa!
Filamu ya familia ya kusisimua ya majira ya kiangazi yenye mapigano makali na visa vya kusisimua vya binadamu, iliyoandaliwa katika ulimwengu ambapo uhalisia pepe ni sehemu ya maisha ya kila siku.
Katika siku zijazo, kila mtu atakuwa na ufikiaji wa OZ, ambao ni ulimwengu wa kidijitali ambapo kila kitu cha ulimwengu wa kweli — kuanzia nyumbani, kazini, shuleni, na kwingineko — kinafanyika mtandaoni. Kenji ni mwanafunzi mwenye kipaji cha hisabati. Akiwa na rafiki yake Sakuma, anafanya kazi ya muda ya kusimamia OZ kupitia kompyuta darasani. Siku moja, Natsuki, msichana ambaye alikuwa amemvutia kwa muda mrefu wakiwa shuleni, anaingia kwa ghafla akitafuta kwa udi na uvumba mtu anayetaka kazi nyingine ya majira ya kiangazi — kutembelea nyumbani kwao Natsuki ili kusherehekea siku ya kuzaliwa ya nyanya yake mkuu, Sakae, ambaye ni kiongozi wa familia yenye nguvu ya Jinnouchi. Kenji hasiti na anajitolea kuandamana naye. Lakini mara tu wawili hao wanapowasili nyumbani, OZ inavamiwa kwa njia ya ajabu na akili mnemba (AI) haramu iitwayo Love Machine. Kenji anaharakisha kurekebisha tatizo hilo, lakini mambo yanazidi kuwa mabaya na familia inakumbwa na msiba wa ghafla. Huku OZ ikiwa hatarini na kidole cha lawama kikielekezwa kwa Kenji, punde anagundua kuwa mhalifu halisi ambaye anahusika na Love Machine ni mtu wa karibu na nyumbani, anayetumaini kuishawishi familia na kubadilisha ulimwengu wote miwili. Filamu hii ya kusisimua ya kisayansi ya SUMMER WARS iliyoongozwa na HOSODA Mamoru, inachanganya mapambano na drama ya kifamilia katika juhudi za kuzuia ulimwengu unaojulikana na kila mtu usiharibiwe.
A SAMURAI IN TIME (2024, 131 min, Comedy)
Ⓒ2024 MIRAIEIGASHA
Radi inamtupa samurai kwa kasi kupitia wakati.
Radi inamtupa samurai mpweke mbele kwa miaka 140 kupitia wakati, na akatua kwenye eneo la filamu inayotayarishwa nchini Japani ya sasa, ambapo kwa makosa anapewa nafasi ya uigizaji kama mshiriki wa ziada katika mfululizo wa tamthilia ya kihistoria.
KOSAKA Shinzaemon, samurai (shujaa wa Kijapani), yuko karibu kumshambulia mwanachama wa ukoo pinzani. Wakiwa wamechomoa panga zao, ghafla anapigwa na radi, na Kosaka anazinduka na kujikuta hayuko tena kwenye Japani ya Enzi za kale, bali yuko katikati ya eneo la kutayarisha filamu ya kisasa ya samurai mjini Kyoto.
Kwa msaada wa mwelekezi msaidizi anayetarajia kuandika hadithi yake ya kihistoria, wanandoa wazee kutoka hekalu lililo karibu, na mwigizaji wa awali wa vitendo hatari katika filamu, Kosaka anazoea haraka jukumu lake jipya kama kirareyaku ambaye ni mwigizaji wa ziada ambaye kazi yake ni kuuawa kwa upanga mbele ya kamera.
Hata hivyo, kadiri muda unavyopita, maisha ya zamani ya Kosaka yanaanza kumrudia. Wakati utayarishaji wa filamu mpya ya kihistoria unapotangazwa, ghafla Kosaka anakutana uso kwa uso na YAMAGATA Hikokuro, ambaye ni Kosaka mpinzani aliyewahi kuapa kumshinda. Samurai hao wa zamani wanapokutana tena wakiigiza bega kwa bega, pambano moja la mwisho la panga linawapa wanaume hao wawili fursa ya kurejesha roho yao ya usamurai, likiwaweka kwenye njia ya upatanisho na kutengeneza filamu mpya itakayopendwa sana. Maisha ya zamani yanakutana na ya sasa katika ucheshi huu mwepesi ulioongozwa na YASUDA Junichi, ukiuliza nini maana ya kuwa samurai katika ulimwengu wa kisasa.
