TANGAZO KWA WAAGIZAJI WOTE WA MAGARI YALIYOTUMIKA KUTOKA JAPAN

2022/3/9

Tafadhali ~Ongea na Ofisi ya JETRO NAIROBI Kwanza~

Shirika la Biashara za Nje la Japan (JETRO) ofisi ya Nairobi {Ofisi ya kanda inayoshughulikia nchi Wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki} inawataka wale wote wanaokusudia kuagiza magari yaliyotumika kutoka Japan, kuwasiliana na ofisi ya JETRO Nairobi kabla ya kujihusisha na wafanyabiashara wa Magari yaliyotumika nchini Japan ili kuepuka hatari ya kutapeliwa.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1957, Ofisi ya JETRO Nairobi imesaidia kuendelea kwa  uwekezaji baina ya Japani na Nchi Wanachama za Afrika Mashariki, na hii imeendelea kukua pamoja na maendeleo ya kiuchumi ya Kanda.

Hata hivyo, kumeshuhudiwa visa kadhaa vya udanganyifu katika uingizaji wa magari yaliyotumika.
Cha muhimu unapofanya biashara, ni kutafuta mshirika anayeaminika. Kwa bahati mbaya, baadhi ya waagizaji hushawishiwa na bei za chini na kutuma pesa nje ya nchi bila ya kudhibitisha uaminifu na hadhi ya muuzaji, jambo linalosababisha uwezekano mkubwa wa kudhulumiwa kwa sababu pesa zinazotumwa kwa wadanganyifu/walaghai hawa haziwezi kurejeshwa.

Kwa hivyo, ofisi ya JETRO Nairobi ingependa kuwahimiza wafanyabiashara wote wa Afrika Mashariki kuwasiliana na ofisi ya JETRO Nairobi kwanza wanapotaka kuagiza chochote kutoka Japan. Ofisi ya JETRO Nairobi itaweza kutambulisha kampuni zinazofaa za Kijapani kwa wote.

Ni muhimu kutambua kwamba ofisi ya JETRO Nairobi ina listi ya kampuni zote zilizoandikishwa nchini Japani na zinazohusika na usafirishaji wa magari yaliyotumika nchini.

Njia salama zaidi ya kuagiza gari lililotumika ni kupitia mfumo wa "JUMVEA Safe Trade". https://www.jumvea.or.jp/jumvea-safe-trade.php

JUMVEA au Muungano ya Wasafirishaji wa Magari yaliyotumika ya Japani, inajumuisha wasafirishaji wapatao 400 wa magari yaliyotumika nchini Japani na kuunganisha waagizaji wa magari yaliyokwishatumika duniani kote na wasafirishaji nchini Japani. JUMVEA inatoa dhamana ya kwamba magari yaliyoagiziwa yatawafikia wanunuzi bila kukosa.

Ofisi ya JETRO Nairobi inasaidia uagizaji wa kila aina ya bidhaa za Kijapani, sio tu magari yaliyotumika. Kwa hivyo, wakati wowote unapotaka kuagiza bidhaa yoyote ya Kijapani, inashauriwa sana upate thibitisho kwa kupitia ofisi ya JETRO Nairobi kwanza.

Ninatumai kwa dhati kwamba kupitia kuendeleza na kuimarisha biashara kwa njia za kuaminika, Japani na nchi wanachama za EAC zitastawi zaidi, na uhusiano wetu wa kirafiki utadumishwa.
Asante sana.

BWANA. SOTARO NISHIKAWA,
Mkurugenzi Mtendaji, JETRO NAIROBI
JETRO Nairobi iko wazi kwa ulimwengu wa biashara na umma kwa jumla kwa mashauriano. Unaweza kuwasiliana nasi kupitia KEN@jetro.go.jp au utupigie simu kwa +254 743 300 460


Ms. Emi MASHIKO
First Secretary, Economic Section, Embassy of Japan in Tanzania
(Email: shomu@dr.mofa.go.jp, Office Tel: +255 22 211 5827/5829)