Onyesho la Makala ya NHK WORLD-JAPAN

2026/5/18
poster
Tumefurahi kutangaza onyesho la makala ya uhalisia katika vyuo vikuu nchini Tanzania. Onyesho hili limepangwa na NHK WORLD-JAPAN, kwa ushirikiano na Ubalozi wa Japan Tanzania
 
Makala yatakayoonyeshwa ni:
"Shajara za Maiko wa Kisasa (Simulizi za Miji ya Nyumbani)"
Katika mji wa Sakata uliopo kaskazini mashariki mwa Japan, maiko wameburudisha watu kwa karne kadhaa. Kwa sasa, mbobezi wa sanaa hiyo anawasaidia mabinti kufuata nyayo zake, na kupata ujasiri kwa kila hatua.
 
Filamu hii itaonyeshwa na tafsiri ya Kiswahili.
Kiingilio ni bure. Usajili si lazima.
 
Tarehe na Ukumbi:
  • 30 Mei (Jumamosi) – Chuo Kikuu cha Ardhi (Dar es Salaam)
  • 6 Juni (Jumamosi) – Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (Morogoro)
  • 7 Juni (Jumapili) – Chuo Kikuu cha Dodoma (Dodoma)
Milango Kufunguliwa: Saa 8:45 mchana / Onyesho: Saa 9:00–9:40 mchana
 
  • 13 Juni (Jumamosi) – Chuo Kikuu cha Zanzibar (Zanzibar)
Milango Kufunguliwa: Saa 7:45 mchana / Onyesho: Saa 8:00–8:40 mchana
 
Tovuti ya NHK Kiswahili (external link): https://www3.nhk.or.jp/nhkworld/sw/