Tamasha la Musimu wa Kiangazi la Jumuiya ya Wajapani 2025

2025/9/24
speech
singing
Mnamo Septemba 20, Tamasha la Musimu wa Kiangazi la Jumuiya ya Wajapani lilifanyika, na Kaimu Balozi Ueda alitoa hotuba.
Tamasha hilo la musimu wa kiangazi liliandaliwa na Jumuiya ya Wajapani nchini Tanzania na lilijumuisha vibanda vya tamasha, maonyesho ya kwaya, na mengineyo. Lilikuwa fursa ya kutambulisha utamaduni wa Kijapani kupitia shughuli kama vile kuvaa yukata (vazi la kitamaduni) na maonyesho ya Bon Odori (ngoma za asili).